Rais JPM Aongoza Viongozi Wakuu Kuaga Mwili wa Mkapa – Pichaz
Global Publishers July 28, 2020 0 Comments
SHARE THIS:
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, iliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Rais Magufuliameongoza hafla ya kumuaga Hayati Benjamin William Mkapa, Rais wa awamu ya Tatu wa Tanzania. Katika hafla hiyo Rais Magufuli ameeleza kuwa Hayati Mkapa ndiye ‘shujaa’ wake na ametangaza rasmi uwanja wa Taifa kuitwa ‘Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifuta machozi wakati akielezea namna alivyomjua Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati akihutubia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akitowa heshima ya mwisho kwa mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Kitaifa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
MSAFARA wa gari maalum ya JWTZ ikiwa imeubeba Mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamin William Mkapoa ukiwasili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutowa heshema ya mwishi kwa Viongozi wa Kitaifa na Wageni waalikwa.
BAADHI ya Wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali Nchini Tanzania wakishiriki katika hafla ya kuuaga Mwili wa Hayati Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Willian Mkapa, iliofanyika Kitaifa leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Rais Mstaaf wa Tanzania wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin Mkapa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwahutubia Wananchi katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo 28/7/2020, katika hafla ya Kitaifa ya kuuanga mwili wa marehemu
BAADHI ya Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao Nchini Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
MJANE wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akitowa heshima yake ya mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa hafla ya Kitaiga ya kuuaga mwili huo iliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan , akitowa heshima ya mwisho kwa mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Kitaifa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa hashima ya mwisho kwa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa marehemu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo 28/7/2020.(Picha na Ikulu)
MSAFARA wa gari maalum ya JWTZ ikiwa imeubeba Mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamin William Mkapoa ukiwasili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutowa heshema ya mwishi kwa Viongozi wa Kitaifa na Wageni waalikwa.
WAGENI Waalikwa na Wananchi na Viongozi wa Serikali na JWTZ wakitowa salute wakati ukipigwa wimbo wa Taifa katika Uwanja wa Taifa Jijini Da es Salaam baada ya kuwasili kwa mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya Kitaifa kwa Viongozi Wakuu kuuaga mwili wa mnarehemu
WAZIRI Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni, akizungumza na kutowa salamu za Nchi yake wakati wa hafla hiyo ya Kitaifa ya kuuanga mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin Willian Mkapa, iliofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam