
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Malaysia, Najib Razak, amekutwa na hatia katika mashtaka saba ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili na kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 na faini ya Dola Milioni 49 (zaidi ya Tsh. 113 Bilioni).
Razak (67) alituhumiwa kutumia fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya mradi wa kimaendeleo katika matumizi binafsi. Anakuwa kiongozi wa kwanza nchini humo kuhukumiwa kwa ufisadi.
Hukumu yake imetolewa siku sita baada ya Mahakama Kuu kuamuru ailipe Serikali Dola Milioni 400 zikiwa ni kodi na faini ambazo hazikulipwa kati ya mwaka 2011 hadi 2017.
Razak ambaye amewahi kutajwa kama mtu mwenye nguvu zaidi nchini humo alikuwa Waziri Mkuu kuanzia 2009 hadi 2018.
Al Jazeera