×

Daktari Mbaroni Tuhuma za Kumpa Mimba Mwanaye

MWANAFUNZI wa Chuo cha Udaktari wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara na mkazi wa Mburahati jijini Dar es Salaam na Itunduma kata ya Mtwango Wilaya na Mkoa wa Njombe,  amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake na kumsababishia ujauzito.

 

Akimsomea mashitaka matano yanayomkabili mshitakiwa huyo Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Matrida Manja,  amesema mshitakiwa Joshua Mhema (26) alitenda makosa hayo katika nyakati tofauti kati ya tarehe isiyojulikana  na shitaka la pili la kubaka alitenda Mei 6 na Mei 26 ,, 2020, na kosa la tatu na la nne la kubaka alitenda Mei 27 ambapo tarehe hiyo  alitenda kosa la kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu .

 

Mshtakiwa alikana mashtaka yote matano ambapo Manja amesema mashtaka yote yanaangukia katika sura ya 130 (1&2) e kanuni ya adhabu na mwenendo wa makosa namba 16 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2016.

 

Manja ameiambia mahakama kuwa makosa yote hayo matano yana dhamana.

 

Kesi  imeahirishwa hadi Agosti 05, 2020,   kwa kuanza kusikilizwa na kutolewa ushahidi.  Mtuhumiwa amepelekwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini.

Leave a Comment