Matukio Mbalimbali Ya Maonesho Banda La Kinondoni Mkoani Morogoro
Global Publishers August 4, 2020 0 Comments
SHARE THIS:
Mkurugenzi mwendeshaji wa Kampuni ya Wasambazaji wa Teknolojia ya Jividudu hai (E.M) kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi. Gigwa Swai akitoa maelezo kwa mtaaalmu kutoka Manispaa ya Temeke katika Banda la Manispaa ya hiyo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Hali ilivyoonekana.Mzee ambaye ni mkazi wa Morogoro, akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Kitengo cha uchaguzi Manispaa ya Kinondoni kuhusu masuala ya uchaguzi alipofika kwenye Banda la Manispaa hiyo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Wananchi waliofika katika Banda la Manispaa ya Kinondoni katika kikundi cha Vijana wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Manispaa hiyo wakiangalia bidhaa za viatu vya ngozi katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Maafisa mifugo Bi. Grace Misonge na Bi Ancila Malamshakutoka Halmashauri ya Chalinze wakipata maelezo kuhusiana na masuala ya Kilimo kwa ujumla.Kikundi Cha wajasiriamali wakinamama kutoka Manispaa ya Temeke waliovaa Tishet za kijivu wakibadilishana ujuzi kutoka Kikundi cha wakina Mama wajasiriamali wa Manispaa ya Kinondoni katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Mfumo wa kuzungusha maji kwa ajili ya ufugaji wa Samaki kwa njia ya kisasa unaojulikana kwa jina la Recirculating Aquaculture System (RAS).