×

Kikongwe Miaka 74 Anaswa Akisafirisha Mabaki ya Mumewe

POLISI  katika uwanja wa ndege wa Munich nchini Ujerumani wamepigwa na mshangao mkubwa wakati wakichunguza sanduku la mbao lililokuwa linasafirishwa na abiria mmoja kikongwe mwenye umri wa miaka 74 ambalo waligundua kuwa lina mifupa ya mume wa mama huyo, maafisa wamesema hapo jana Jumanne.

 

Maafisa wa forodha, daktari na waendesha mashitaka waliitwa, na kusema kuwa hakuna uhalifu uliofanyika katika kitndo hicho, shirika la habari la Ujerumani (DPA) limeripoti.

 

 

Baada ya kumhoji mwanamke huyo na mwanaye wa kike mwenye umri wa miaka 52, polisi waligundua kuwa wanawake hao wawili walikuwa safarini kutoka Ugiriki kwenda katika nchi walikozaliwa ya Armenia kupitia Munich na Kiev.

 

Polisi wamesema mama huyo alisema mume wake alifariki mwaka 2008 na alizikwa mjini Thessaloniki, Ugiriki,  na kwamba yeye na mtoto wake wa kike waliamua kurejesha mabaki hayo nyumbani nchini Armenia.

 

Leave a Comment