
Rais Emmerson Mnangagwa ameapa kupambana vikali na wapinzani na wanaharakati baada ya kuongezeka kwa maandamano. Pia, amevishutumu vyama na nchi za kigeni kufanya uchokozi dhidi ya utawala wake.
Rais Mnangagwa aliingia madarakani akiwa ametoa ahadi ya kufanya mabadiliko lakini wakosoaji wanamuona anafanya utawala wa mabavu, matumizi mabaya ya fedha kama ilivyokuwa kwa Rais Mugabe.
Wanaharakati wanamuona kuwa ni Rais mkali zaidi kuliko hayati Mugabe. New York Times imeripoti kuwa wanaharakati na wapinzani walioshtakiwa kwa uhaini ndani ya utawala wa Rais Mnangagwa ni wengi kuliko kipindi cha Mugabe.
Ofisi ya Kamishna wa Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Haki za Binadamu imesikitishwa na jinsi Zimbabwe inavyotumia #COVID19 kama kisingizio cha kubana uhuru wa raia.