
Klabu ya Yanga leo Agosti 12, 2020 imetangaza kuingia kambini rasmi Jumatatu Agosti 10, 2020 kujiandaa na msimu mpya.
Taarifa iliyotumwa klwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa klabu hiyo, timu ya Wananchi itaingia kambini kuanza maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza Septemba 6
Hadi sasa Yanga ndiyo klabu ambayo imeachana na wachezaji wengi baada ya dirisha la usajili kutangazwa Agosti Mosi kuliko klabu zingine za Ligi Kuu, wakiwa na lengo la kuboresha kikosi chao kiweze kuleta ushindani zaidi msimu ujao.
Wachezaji waliosajiliwa na kutangazwa rasmi na Yanga mpaka sasa ni Wazir Junior kutoka Mbao, Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union, Zawadi Mauya kutoka pamoja Kagera Sugar, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Yassin Mustapha kutoka Polisi Tanzania wachezaji wote wakiramba kandarasi ya miaka miwili.
Nyota walioachwa huru ndani ya kikosi hicho ni Mrisho Ngasa, David Molinga, Jaffar Mohamed, Tariq Seif, Andrew Vicent, Papy Kabamba na Mohamed Banka.