×

Maambukizi Virusi vya Corona Afrika Yafikia Milioni 1

ZAIDI ya watu milioni moja wameambukizwa virusi vya Corona barani Afrika.

 

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la AFP, Afrika imerekodi maambukizi 1,000,054 huku  watu wapatao  21,724 wakifariki kutokana na ugonjwa huo wa Covid-19.

 

Idadi ya maambukizi hayo ni asilimia tano tu ya maambukizi yaliyorekodiwa duniani kote. Vilevile, idadi ya maambukizi huenda ikaongezeka kutokana na hofu ya kutokea kwa wimbi la pili la mlipuko wa virusi hivyo licha ya baadhi ya mataifa kuonekana kufikia kilele cha maambukizi.

 

Kwa mujibu wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika (ACDC) nchi tano barani Afrika zimerekodi asilimia 75  ya maambukizi yote barani humo.

Leave a Comment