×

Kisa Yanga SC, Mrundi Agoma Kubaki Namungo

NAELEZWA kuwa mshambuliaji wa Namungo FC, raia wa Burundi, Bigirimana Blaise, amekataa kuongeza mkataba wa kukipiga ndani ya klabu hiyo ili kutimiza ndoto zake za kujiunga na Yanga.

 

Taarifa za kuaminika kutoka kwa mtu wa karibu na Blaise zilisema, nyota huyo aliyemaliza ligi akiwa na mabao 11, amekuwa akimshinikiza meneja wake kufanya mpango wa kumtafutia nafasi ya kusajiliwa na Yanga, kwa kuwa ndoto zake kubwa ni kuona msimu ujao anavaa jezi ya timu hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, chan-zo cha kuaminika kutoka ndani ya Namungo, kilisema: “Bigirimana amegoma kuongeza mkataba wa kubaki hapa Namungo kwa sababu tamaa yake kubwa ni kwenda kuichezea Yanga, amekuwa akisisitiza muda mrefu kuwa anatamani kuwa mchezaji wa timu kubwa kwa msimu ujao.”

 

Championi Jumamosi lilimtafuta Bigirimana mwenyewe ili kutaka kujua chochote juu ya ishu hiyo ambapo alisema: “Kiukweli nataka kupata changa-moto mpya msimu ujao, nimegoma kuongeza mkataba Namungo kwa sababu nataka kucheza timu ny-ingine. Masuala ya Yanga si-wezi kusema, kama kweli yapo basi meneja wangu atakuja kuweka wazi.”

STORI: ISSA LIPONDA,DAR ES SALAAM

Leave a Comment