×

Harmo Aanika Siri Nzito ya Wolper ‘Alimtaka Mondi Kimapenzi’ – Video

 

STAA wa muziki kutoka Umakondeni, Harmonize hatimaye amevunja ukimya na kuamua kuanika siri nzito iliyokuwa moyoni mwake kwa miaka kuhusu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye pia ni msanii wa Bongo Movies, Jackline Wolper.

 

Akizungumza wakati akipafomu kwenye Jukwaa la Jipozee usiku wa kuamkia leo, Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Harmonize amesema miongoni mwa sababu zilizopelekea kuachana na Wolper ni kumfumania na meseji tofauti tofauti za wapenzi wake akiwemo mmoja aliyekuwa China na mwingine Burundi.

 

Lakini kubwa kuliko, Harmonize amedai kuwa Wolper alikuwa akimtaka Diamond kimapenzi na alimwandikia meseji akimwahidi mahaba matamu pamoja na kumzalia mtoto wa kiume.

 

“Sijawahi kusema popote pale leo ndio nasema ili ajue, yeye mwenyewe hajui kama mimi najua. Wolper alikuwa akimtaka Bosi wangu za zamani, Diamond kimapenzi, akawa anamtumia meseji Diamond akimwambia kwamba ‘nitakuzalia mtoto wa kiume’ kipindi hicho Diamond anamtoto mmoja Latiffah.

“Akawa anamwambia Diamond, ‘Nipo na Harmonize nipate ukaribu tu nawewe’, Diamond aliniita mdogo wangu njoo, alishindwa kuniambia live, ikabidi anywe pombe kwanza ndipo aweze kuniambia kwamba mwanamke wako ananitaka kimapenzi.”

 

“Nilipanga nisimwambie lakini anasema vingi. Unavyomwita mwanamke wangu (Sarah) sponsor ambaye nampenda, kibinadamu inaumiza. Inaniumiza kumwita mpenzi wangu Sponsor ambaye punde si punde tunatarajia kuwa na mtoto kwa sababu Sarah ni mjamzito.

 

“Siku moja tulikuwa kwenye shoo, nimekaa naye back stage, ghafla ikaingia simu ya mwanaume mmoja amemsevu ‘My Love’, alikuwa bwana’ake wa sasa Rich Mitindo, nikainyakua simu nikakimbia nayo, bahati zuri nikaona chumba nikaingia, nikapekua simu nikakuta meseji za huyo mwanaume alikuwa China anamlalamikia kwamba amemtenga ananijali mimi kitoto chake, mimi mwanaume mzima najitahidi kutafuta riziki nimtunze naitwa kitoto?

 

“Nikaendelea mbele zaidi nikakuta meseji za bwana’ke mwingine yupo Burundi, iliniuma sana…. Mpenzi wa sasa wa Wolper ambaye ni Rich Mitindo alianza kutoka na Wolper muda mrefu tangu nikiwa naye kwenye mahusiano. Baada ya kupitia mkasa huo, niliingia studio na kuandika wimbo wangu wa #Nishachoka. Wimbo huu ulikuwa maalum kwa Wwolper,” amesema Harmonize.

 

Leave a Comment