×

Samia Afungua Mkutano Baraza Kuu UWT – Video

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika  Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dodoma leo Agostui 10, 2020.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa jukumu la kulainisha mitambo ya uchaguzi kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekabidhiwa kwa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT).

Amesema hayo wakati akihutubia Baraza Kuu la Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa White House mjini Dodoma, ambapo amesema kuwa jukumu la kampeni ni jukumu zito.

…Akimtunuku Tuzo Maalum Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu,  kwa kutambua mchango wake na kuwawakilisha wanawake vizuri katika majukumu yake.

“Jukumu hili ukilichambua kiundani ni jukumu zito sana kujitoa na kujitolea kwa sababu kazi tunayokwenda nayo  ya kuanza ya kampeni si kazi nyepesi, ” amesema.

Amesisitiza  kuwa inahitaji uadilifu na umakini mkubwa kwani Chama Cha Mapinduzi ni kikubwa na kinahitaji ushindi mkubwa.

 

Leave a Comment