×

Yanga Waigomea Hukumu ya Morrison

 

UONGOZI wa Yanga kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii umetoa taarifa kuwa haujaridhishwa na uamuzi huo na watakata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) muda mfupi baada ya winga Bernard Morrison kutangazwa kushinda shauri na kuwa mchezaji huru dhidi ya waajili wake wa zamani Yanga, uongozi wao umesema watakata rufaa.

 

Mwenyekiti wa kamati ya Hadhi, Sheria za Wachezaji, Elias Mwanjala alitangaza hukumu hiyo baada ya sakata hilo kuchukua siku tatu likisikilizwa.

Yanga wamesema wanasubiri nakala ya hukumu kutoka kamati husika ili waanze kuchukua hatua.

Leave a Comment