×

Dkt Abbas: Tutaweka Rekodi ya Umeme Vijijini – Video

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas, leo Agosti 15, 2020, amesema ifikapo Juni 30 mwakani, vijiji vyote vitakuwa na umeme.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam akielezea utekelezaji uliofikiwa katika sekta ya madini  na sekta ya nishati nchini alipowaambia waandishi wa habari kamba hivi sasa nchi ina jumla ya megawati 1,602.32 kutoka megawati 1,308 za mwaka 2015.

Amesema hiyo imetokana na kazi ya Rais John Magufuli mnamo miaka mitano ambapo pia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita alikuwa kiongozi wa   Jumuiya ya Maendeleo  ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

 

Serikali ya Dkt Magufuli pia imetumia takribani TZS Trilioni 1.109 ya fedha za ndani kutekeleza miradi mikubwa miwili ya umeme wa gesi: Kinyerezi-I Extension megawati 185 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na zaidi ya TZS Bilioni 315.4

Sehemu ya maelezo aliyoyatoa Dkt. Abbas kuhusu mafanikio hayo ni ifuatayo:

Jumla ya TZS Trilioni 2.29 zimetumika ambapo kati ya fedha hizo, TZS Trilioni 1.78 ni fedha za ndani na TZS Bilioni 515.71 ni fedha za nje kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.

 

Hadi kufikia Julai, 2020 jumla ya vijiji 9,412 vimeunganishwa kutoka vijiji 2,018 mwaka 2015, ikiwa ni sawa na ongezeko la vijiji 7,394.

 

Aidha, zaidi ya magari 400 yamefungwa mifumo ya matumizi ya gesi asilia ikilinganishwa na magari 60 yaliyokuwa yameunganishwa mwaka 2015

 

Aidha, Serikali inaendelea na taratibu za malipo kwa wananchi waliobaki na kuendelea na majadiliano ya Mkataba Hodhi (Host Government Agreement – HGA) na Kampuni zitakazotekeleza mradi. Hii itasaidia usafirishaji wa gesi kwenda nje. Serikali inaendeleza ujenzi wa mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia (Liquefied Natural Gas – LNG). Mradi huu unalenga kusindika gesi asilia kuwa kimiminika. Jumla ya TZS Bilioni 5.2 imelipwa kwa wananchi 618 kati ya 693 watakaopisha mradi katika eneo la Likong’o, Lindi

 

Kuna kazi kubwa imefanyika katika mageuzi kwenye Sekta ya Madini. Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa

 

Kazi zilizokamilika ni pamoja na tafiti mbalimbali za Kijiolojia, kijiofizikia na Kijioteknikia na kukamilika kwa kazi ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira. Aidha, utwaaji wa ardhi katika maeneo ya miundo (Tanzania imetenga Bilioni 1 ya fidia).

 

Faida kubwa ni kuongezeka kiwango cha madini yanayojulikana kuwa yamezalishwa na kuongezeka kwa mapato ya Serikali – Dkt. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali

 

Moja ya mafanikio ya Magufuli katika Sekta ya Madini hadi Juni, 2020, jumla ya masoko ya madini 31 na vituo vya ununuzi wa madini 39 vilianzishwa maeneo mbalimbali nchini.

 

Kisa cha mchimbaji mdogo Saniniu LaIzer ambaye Juni 24, 2020 aliishangaza dunia baada ya kuiuzia Serikali Madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 9.27 na kisha akapata jiwe la kilo 5.80 ni ushuhuda wa mafanikio ya Ukuta wa Mirerani

 

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kuweza kupatikana kwa madini ya Tanzanite yenye uzito na thamani hiyo kubwa ambayo yaliiwezesha Serikali kupitia Tume ya Madini kukusanya maduhuli ya Shilingi 881,348,298.25 na ni matokeo ya usimamizi imara

 

Saniniu aliuza mawe hayo yakiwa na jumla ya thamani ya TZS 7,744,152,703.82. Pia Agosti 3, 2020 mchimbaji huyo aliiuzia Serikali Tanzanite nyingine yenye uzito wa kilo 6.3317 ambayo ilikuwa na thamani ya Shilingi 4,846,537,271.12.

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment