×

Chama Amvuta Shonga Simba

KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Clatous Chama, amefunguka kuwa Mzambia mwenzake, Justin Shonga, anaweza kutua klabuni hapo endapo mabosi wa klabu hiyo wataweka usiriazi katika kuinasa saini yake.

 

Chama ameongeza kuwa, Shonga anayekipiga Orlando Pirates ya Afrika Kusini, anaweza kusaini Simba kwa msimu ujao ikiwa tu mabosi hao watampatia kiasi kizuri cha fedha kitakachomfanya atue hapo.

 

Mabosi wa Simba wamekuwa wakimfutilia Shonga kwa ajili ya kumshusha kikosini hapo kwa msimu ujao.

Chama amesema kuwa hakuna tatizo lolote kwa Shonga kutua Simba kutokana na yeye kuwa mchezaji na anaweza kucheza sehemu yoyote.

 

“Juu ya Shonga kuhitajika Simba kwangu naona anaweza kuja kucheza kwa sababu yeye ni mchezaji na anaweza kucheza kokote pale.

“Kitu muhimu ni kwa viongozi kuwa naye siriazi na kumpelekea dau ambalo litamfanya atue na kucheza hapa,” alimaliza Chama.

SAID ALLY, Dar es Salaam

 

Leave a Comment