RAIS wa Barcelona, Josep Bartomeu, amethibitisha kuwa Ronald Koeman atapewa kibarua cha kuwafunza miamba hao wa Catalan. Kwa sasa Koeman ni kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, lakini Agosti 18 alikwenda Barcelona kukamilisha dili hilo na anatarajiwa kutangazwa juma hili.
Klabu ya Barcelona jana ilitangaza kumfuta kazi kocha wake, Enrique Setién Solar, ikiwa ni siku chache baada ya kuondolewa kwa aibu kwenye mashindano ya Klabu Bingwa barani Ulaya kwa kipigo cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munchen.
Kuhusu uvumi kwamba nyota wa klabu hiyo, Lionel Messi, ataondoka, Bartomeu amesema, “Messi anataka kumalizia soka lake Barca, na amelisema hilo mara nyingi… Bado ana mkataba hadi 2010.”
Pamoja na hatua hiyo mpya, pia amedokeza kwamba timu yake itajengwa upya kwa upande wa wachezaji.
