MWANAMKE mmoja nchini Kenya anatuhumiwa kumuua na kumzika mtoto wa siku moja baada kulaumiana na mume wake juu ya kupata mimba nje ya ndoa.
Mume wa mwanamke huyo ambaye amekuwa mbali na mkewe kwa majukumu ya kikazi kwa zaidi ya mwaka, alishangazwa kusikia mkewe anatarajia kujifungua, hivyo alimpigia simu na kuulizia jambo hilo.
Mwanamke huyo aligundulika na shemeji yake ambaye alimripoti na walipombana alisema kuwa amemzika mtoto huyo kwenye shamba la mihogo, lililokuwa karibu na nyumbani kwao.
Mtoto huyo amezikwa kwa mara ya pili kwa heshima, na mwanamke huyo amekimbia baada ya kujua kuwa anatafutwa.
