UONGOZI wa Klabu ya Azam, umesema leo kwenye kilele cha Azam Festival, mbali na kuwatambulisha wachezaji wapya, pia kutakuwa na burudani mbalimbali pamoja na sapraizi za kutosha.
Leo Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar, Azam FC itatambulisha wachezaji wake itakaowatumia msimu ujao wa 2020/21 pamoja na jezi zao watakazotumia.
Ofi sa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Azam FC ni timu kubwa na bora, hivyo malengo makubwa ni kuifanya izidi kuwa imara, mashabiki wanapaswa kuendelee kuipa sapoti timu yao na kujitokeza kwa wingi kwenye kilele cha Azam Festival.”
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alisema kuwa watafanya mambo mengi mazuri huku burudani ikitolewa pia kutoka kwa msanii maarufu wa Muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba na wasanii wengine akiwemo Msaga Sumu.
Kiba alisema: “Nimefurahi sana kupata nafasi ya kutumbuiza mbele ya mashabiki, mimi ni mwanamichezo. Ninapenda kuwaambia watu kwamba waje kwa wingi, watu wa mwanzo kabisa watakaonunua jezi kwa shilingi 20,000 nitasaini na kupiga nao picha.”
Katika tamasha hilo ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, zitachezwa mechi mbalimbali za utangulizi, kisha itafuatiwa na mechi rasmi ya kirafi ki kati ya Azam FC dhidi ya Namungo FC.
Kwa mara ya kwanza, mashabiki wa Azam watawashuhudia nyota wao wapya waliosajiliwa hivi karibuni ambao ni Awesu Awesu, Ally Niyonzima, Ayoub Lyanga, Ismail Kada, David Kissu, Emmanuel Charles na Prince Dube

