×

Diamond Alivyotua na Chopa Uwanja Mkapa (Picha +Video)

STAA wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Daimond Platnumz’  Agosti 23, 22020 ameuteka Uwanja wa Mkapa, takribani dakika tano, alizoingia na helkopta kutumbuiza tamasha la ‘Simba Day’.

usafiri wa helkopta akiwa sambamba na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.Wakati Diamond akitoa burudani hiyo ya nguvu akiimba nyimbo mbalimbali ikiwemo ya kuisifia Simba inayoitwa Simba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ alishindwa kujizuia na kuungana naye.Diamond alipomaliza kupiga shoo, akaondoka eneo la tukio na usafiri aliokuja nao.

Kumbuka Diamond alipiga shoo hiyo kwa takribani dakika 30, kuanzia saa 10:24 hadi 10:54 jioni, huku akiwa na madansa 68

Leave a Comment