UONGOZI wa Namungo FC, umeweka wazi kuwa ndani ya wiki hii wamepanga kuwafanyia sapraizi mashabiki wake waliopo Arusha kwa kutambulisha nyota watatu wapya kabla ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
Leo Alhamisi, Namungo FC inatarajiwa kuwasili jijini hapa tayari kwa mchezo huo utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.Ofisa Habari wa Namungo FC, Kindamba Namlia, ameliambia Spoti Xtra kuwa:
“Tumewaandalia sapraizi ya kutosha Wanaarusha, tutawatambulisha wachezaji wapya watatu, pia jezi tutakazotumia msimu wa 2020/21. Kikubwa watu wajitokeze siku ya mechi kutuunga mkono.
Stori: Kennedy Lucas, Arusha
