×

Samia Apokea Wapinzani 150 Tandahimba

Mgombea mwenza wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi  Ilani ya CCM ya 2020/25 Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Mahuta Tandahimba,  Katawi Ahmad Katawi,  ili kuinadi kwenye mikutano ya kampeni ya  CCM leo Septemba 11, 2020.

MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 11, 2020 amezungumza na wananchi wa Jimbo la Mahuta, Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara,   kwenye mkutano wa kampeni wa CCM kijijini Mahuta, Mtwara, leo Septemba 11, 2020.

Wanachama 150 kutoka vyama vya ACT Wazalendo, CUF na Chadema wilayani Tandahimba, leo wamerudisha kadi  za vyama vyao na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa huo wa kampeni.
…Akiagana na wanachama hao wa CCM, Mahuta, Tandahimba.
Baadhi ya wanachama waliorudisha kadi za vyama vyao na kujiunga na CCM.

Leave a Comment