
Meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platniumz’ jana alisababisha mafuriko makubwa ya watu wakati akizindua kampeni zake za kutetea kiti chake cha Udiwani wa Kata ya Kilungule, Mbagala Jijini Dar.

Katika uzinduzi huo Mkubwa Fella alimwaga sera zake huku akieleza mambo mengi aliyoyafanya kipindi chake kilichopita ikiwemo kuongeza madarasa kwenye shule za msingi na sekondari pamoja na ujenzi wa shule ya Msingi Martin Lumbanga ulipofanyika uzinduzi huo.

Mengine ni uchimbaji wa visima na kumaliza shida ya maji kwenye kata hiyo, ujenzi wa barabara za mitaa na mengineyo.

Pamoja na utamu za sera hizo, uzinduzi huo ulinogeshwa na wasanii mbalimbali wa bongo fleva, taarab na ngoma za asili.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL