×

JPM: Muleba Mna Mabishano Yenu Yanawapa Shida – Video

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amewaonya wananchi wa Muleba Kusini kuacha makundi na kuwachagua wagombea wa CCM ili wakawaletee maendeleo.

 

Magufuli amesema hayo leo Jumanne, Septemba 15, 2020, wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kasharunga akiwa katika kampeni zake za kuwania urais ambapo ameingia mkoani Kagera.

 

“Kipindi kilichopita bahati mbaya hapa hamkumpa kura diwani wa CCM, lakini sisi CCM tuna uvumilivu, tukatoa milioni 500 tukajenga hospitali pale, nasikia huyioaliyekuwa diwani wa hapa anasema aliileta yeye. Tuliamua kuijenga kwa sababu tuliona wananchi wa hapa wanateseka sana, mlinichagua mimi na Dkt. Tibaijuka kwa kura nyingi sana, huwezi kuwahukumu watu wa hapa kwa kosa dogo wanawake wakateseka kujifungua.

 

“Kosea kuoa unaweza ukampa talaka mkeo lakini usikosee kuchagua, madhara yake ni makubwa sana. kulikuwa na Masilingi hapa akiwa mbunge, mkawa mna gomagoma, lakini nikamteua akawa balozi Marekani, amefanya kazi kubwa.

 

“Ndugu zangu wa Muleba nawaeleza, matatizo yenu madogomadogo yanawasababisha mnakuwa na matatizo makubwa, mabishano yenu ya chinichini ndiyo yanawapa shida. Saa nyingine mnanipa shida namna ya kuhudumia majimbo, unakuta diwani wa pale unasema CCM oyee anakunyoshea vidole viwili utadhani anataka kukupiga na manati.

 

“Wakati wa mchakato wa kura za maoni palikuwepo na wa kwanza, wa pili, wa tatu mpaka wa miwsho, sisi CCM tuna macho, Kamati Kuu ilivyoketi ikasema atakayeleta maendeleo ya ukweli kwa Muleba ni Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo (Muleba Kusini), mpeni kura kijana wenu,” – Dkt. Magufuli.

 

Leave a Comment