
Jumla ya watoto 150 wa Shule ya Msingi Nzasa iliyopo mkoani Pwani wamepewa taulo za kike (Pedi) kutoka katika shirika la NANTAMBALELE FOUNDATION.
Akizungumza mapema leo ,wakati wa ugawaji wa taulo hizo, muasisi na Mkurugenzi wa shirika hilo, Shakira Salumu amesema kuwa Kazi wanazozifanya kwenye jamii, ni kuzifikia familia duni, walemavu, wagonjwa wa muda mrefu, wazee, yatima, wajane na yeyote yule anayehitaji msaada wa aina mbali mbali kama vile, afya, lishe, mavazi, elimu, nk.

“Katika kwa kipindi hiki tupo na Project iitwayo SCHOOL DADAZ, ambapo tunashirikiana na TUKUZA FOUNDATION.
Hii tunadili na wanafunzi wa shule za msingi kwa lengo la kuwapa elimu ya mabadiliko ya hedhi na kuwapatia pedi.

“Tumefanikiwa kuongea na watoto zaidi ya 150 ambao kati ya hao 53 ni yatima, na wanaoishi katika mazingira magumu japo wengine wanaoishi na wazazi wao lakini wana changamoto hivyo tunawapatia madaftari na vifaa vya shule kiujumla.
“Na huwa tunafanya project tofauti tofauti kulingana na hali, ili tujalibu kugusa kila sehemu ya tatizo kwenye jamii.

“Tunaomba na kukushauri jamii kuunga mkono, serikali, mashirika, taasisi, hata mtu mmoja mmoja anaeonesha kuthubutu kufanya ukombozi ndani ya jamii.
Pia tusikubali kuishi na mtu mwenye tatizo lolote ambalo wewe unaweza kumsaidia au kumtafutia msaada. “alisema Shakira.