×

Rais Aomba ‘Jerusalema’ ya KG Ichezwe Kwenye Sikukuu

 

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amewaomba raia wa nchi yake kusherehekea siku ya Urithi ya Mwaka huu (Heritage Day) kwa kufanya shindano la densi ya wimbo wa Jerusalema.

 

Jerusalema ni wimbo wa mwanamuziki wa Afrika Kusini  ambao umevuma na kusambaa kote duniani. Wimbo huo ulinadi densi ya aina yake inayochezwa na makundi ya watu kote duniani ambayo inasambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.

 

Heritage Day ni sikukuu inayosherehekewa kila mwaka tarehe 24 Septemba kwa ajili ya maadhimisho ya utamaduni na utofauti wa watu wa nchi hiyo.

 

“Hapawezi kuwa na njia nyingine nzuri ya kusherehekea utaifa wetu kuliko kujiunga na jambo ambalo linasambaa kote duniani ambalo ni densi ya Jerusalema Challenge,”  Ramaphosa alisema katika hotuba yake ya televisheni.

 

“Kwa hiyo , ninawaomba nyote kushiriki  Siku ya Urithi- Heritage Day — na muonyeshe dunia kile tunachoweza kukifanya.”

 

Leave a Comment