×

Ujenzi Kituo cha Mabasi Mbezi Wafikia Asilimia 80

UJENZI wa Kituo cha Mabasi cha Kimataifa cha Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, umekamilika kwa asilimia 80, hii ikimaanisha bado kazi ndogo tu ya kumaliziwa kabla ya kuanza kutumika rasmi na kutoa fursa za ajira mbalimbali na biashara.

 

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo ambao una lengo la kuongeza ajira kwa vijana wengi huku akibainisha kuwa stendi hiyo imejengwa kutokana na ile ya Ubungo kuzidiwa uwezo, hivyo imekuwa ndogo kulinganisha na mahitaji ya watu.

 

Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa Kunenge, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, alieleza ujenzi huo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 50 za Tanzania, fedha zilizotolewa na serikali kuu kwa ajili ya mradi huo wa kimkakati.

Leave a Comment