×

Benki Ya NCBA Yazindua Matawi Mapya Mawili Arusha Leo

Mkurugenzi Mtendaji na CEO wa Benki ya NCBA Margret Karume (kulia) mwenye bendera na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa, Wafanyabiashara wadogo na wa kati wa benki hiyo, Gift Shoko wakiwa kwenye maandamano ya uzinduzi huo.

Benki ya NCBA Tanzania Limited (NCBA) imefanya uzinduzi wa kihistoria wa matawi yao mawili mapya jijini Arusha leo tarehe 19 Septemba, 2020.

Bendi ya polisi ikitumbuiza kwenye maandamano hayo.

Matawi hayo mawili mapya ya Arusha ni Tawi la Clock Tower lililopo Fire Road, Jengo la TFA na Tawi la Sokoine lililopo Barabara ya Sokoine, Central Plaza ghorofa ya chini.

Sehemu ya wakazi waliojitokeza wengine wakiwa kwenye baiskeli.

Benki ya NCBA ni muunganiko wa hiari kati ya NIC (T) Limited na CBA Bank (T) Limited ambapo huduma rasmi za taasisi hii mpya ya Kifedha zilianza Julai 8, 2020 baada ya idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Mmoja wa waheshimiwa akiwapongeza maofisa wa benki hiyo baada ya uzinduzi huo.

Leave a Comment