Chopa pamoja na magari yanayotumika katika kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) yakiwa tayari.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeonyesha chopa ambayo kimepanga kuitumia kwenye awamu nyingine ya mwendelezo wa kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao.
Hii imekuja ikiwa ni siku kadhaa tu Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally kusema; “Tutakuwa na mizunguko sita ya kampeni, tumemaliza round ya kwanza sasa tunaingia round ya pili ambayo itakuwa nzito kuliko ya kwanza, tukifika awamu ya sita tutafahamiana zaidi.”
Leo Septemba 21, 2020, chopa hiyo na magari ya mgombea urais wa chama hicho, John Magufuli, yamefika Urambo mkoani Tabora tayari kuendelea na kampeni hizo.

View this post on Instagram
View this post on Instagram


