×

Lori la Mafuta Lawaka Moto Morogoro

 

JESHI la Zimamoto na Uokoaji mkoani Morogoro limefanikiwa kuudhibiti moto wa mafuta kutokana na gari lenye namba za usajili T862 BZS na tela namba T814 DBZ kushika moto katika eneo la Kiegea, wilayani Kilosa.

 

Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi hilo mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF), Goodluck Zelote,  hakukuwa na madhara yoyote kwa binadamu na chanzo cha moto huo hakikujulikana mara moja ila inasadikika ni hitilafu katika mfumo wa umeme wa gari hilo.

 

Leave a Comment