JUMLA ya majeneza 27 yaliozikwa zaidi ya miaka 2,500 iliyopita yamefukuliwa na wanaikolojia katika makaburi ya zamani nchini Misri.
Majeneza hayo yalipatikana katika kisima kipya kilichogunduliwa katika eneo moja takatifu lililopo huko Saqqara, Kusini mwa Mji mkuu wa Cairo. Saqqara lilikuWa maziko ya watu wengi kwa zaidi ya miaka 3,000 na limeorodhedhwa miongoni mwa turathi duniani.
“Utafiti wa awali unaonYesha kwamba majeneza hayo yalikuwa yamefungwa kabisa na kwamba hayajawahi kufunguliwa tangu yalipozikwa, alisema Waziri wa Mambo ya Kale nchini Misri, Khaled al-Anani.
al-Anani amesema awali alichelewesha kutangaza ugunduzi huo hadi pale alipotembelea eneo hilo mwenyewe, ambapo aliwashukuru wafanyakazi kwa kufanya kazi katika hali ngumu chini ya kisima hicho chenye urefu wa mita 11.
Uchimbuaji unaendelea katika eneo hilo huku wataalamu wakijaribu kujua maelezo zaidi kuhusu chanzo cha majeneza hayo. Wataalamu wanasema kwamba majeneza hayo yalikuwa hayajafunguliwa tangu yalipozikwa
Waziri huyo alisema kwamba alitumai kwamba ugunduzi huo utazidi kufumbua ‘siri zaidi’ katika mkutano na wanahabari katika sku zijazo. Vitu vingine vya kale vilivyogunduliwa karibu na majeneza hayo ya mbao pia vilionekana vimeundwa kwa mandhari mazuri na kupakwa rangi za kuvutia.
Mnamo mwezi Novemba 2018, kiwango kikubwa cha wanyama waliokaushwa na kuhifadhiwa karibu na Saqqara walionYeshwa kwa umma kwa mara ya kwaNza. Ugunduzi huo ulihusisha paka, mamba, nyoka aina ya kobra na ndege.
Eneo la Saqqara, lililopo kilomita 30 kusini ma mji wa Cairo , ni eneo lenye makaburi ya zamani ambalo pia lilikuwa likihudumu kama eneo la maziko la mji mkuu wa zamani wa Misri Memphis, kwa zaidi ya miongo miwili. Katika miaka ya hivi karibuni , Misri imezidisha ukuzaji wake wa ugunduzi wa vitu vya kale kwa lengo la kufufua utalii wake.
