CELINE NJOKI (34), ni mama wa watoto watatu nchini Kenya. Ni vigumu sana kwa mtu kuweka akilini mwake mahangaiko na uchungu mwingi ambao mama huyu amepitia katika miaka yake duniani.
Usiku mmoja mwezi Juni, mwaka wa 2016 hatasahau wakati ule mama huyu wa watoto watatu hakuwa na makazi ya kuish alikuwa analala mitaani katika nyumba moja iliyokuwa mahame.
Anakumbuka usiku wa manane alivamiwa na wanaume aliowahesabu hadi 15 wote walimbaka mmoja baada ya mwingine na kumuacha akiwa ameumizwa sehemu za siri kiasi cha kuhitaji upasuaji ambapo alihitaji kushonwa mara kadhaa ili aweze kwenda haja zake kama kawaida.
Mama huyo anasema kuwa anashuku kuwa wanaume hao walikuwa wezi waliokuwa wametekeleza uhalifu sehemu fulani na walikuwa hapo kugawa mali ya wizi. Ndipo wakamvamia akiwa amelala.
Baada ya mkasa huo, ilibidi asaidiwe na wasamaria. Alipata matibabu pia kiakili kutokana na unyama aliyofanyiwa na kwa msaada wa rafiki alimtambulisha kwa shirika la kuwasaidia wanawake lililompangia nyumba na kumsaidia kwa ajira.
Maisha yalionekana kurudi kama kawaida na alihisi kuwa angeyasahau yaliomfanyikia ila mengi yalikuwa yanamsubiri mbele.
Siku moja mnamo mwezi Desemba mwaka wa 2017 alipokuwa anatoka kazini jioni alivamiwa tena akiwa barabarani na wanaume aliowahesabu kuwa sita wote walimbaka mmoja kwa mwengine. Maumivu na nyuzi za kale zote ziliraruka kutokana na kasi ya ubakaji.
“Hawa walionibaka hawakuniibia chochote, ninashangaa kwa kuwa haikuwa usiku lakini walifaulu kunishika kwa nguvu baada ya kumaliza walichokifanya waliniacha hapo nikiwa hoiambapo nilimpigia simu rafiki wangu aliyekuja kuniokoa alinipeleka hospitalini,” anakumbuka Celine.
Celine alifanyiwa upasuaji mwengine sehemu za haja kubwa kwa kuwa alikuwa ameharibiwa tena wakati wa ubakaji. Ubakaji wa mwisho kilimtoa moyo wa kuendelea na maisha yake kwani alianza kujiuliza ni kwa nini anakuwa muathiriwa wa ubakaji kila wakati?
Baada ya miezi minne, Aprili mwaka wa 2018 ubakaji mwengine ulimkuta
“Walivunja nyumba yangu wakati wa usiku na wanaume hao walikuwa wamevalia barakoa lakini nadhani kuwa ni walewale walionibaka barabarani kwani nilizifahamu sauti zao na hata kunusa manukato waliokuwa nayo ,” anakumbuka Celine.
Vilevile, alianza kuwa na woga wa kutembea pekee yake kwani alikuwa na wasiwasi kila mara alipokuwa anakutana na wanaume barabarani.
Celine anasema kuwa mikasa hiyo iliripotiwa katika vituo vya polisi lakini hadi sasa hakuna hata mmoja amekamatwa.
Celine Njoki alizaliwa katika mazingira ambayo ndoa kati ya wazazi wake haikudumu. Mwanadada huyu anakumbuka akiwa na miaka minne hivi mamake aliondoka na kakake aliyekuwa mdogo na tangu wakati huo Celine hakuwahi msikia wala kumuona mama yake.
Baba yake Celine alifanya kila awezalo kuwapa watoto wake mapenzi ya mama na ya baba na maisha ya kawaida Celine alipohitimu miaka saba, baba alifariki na hakuna aliyejitolea kuwafariji kwa kupoteza baba. Anachofahamu ni kuwa ghafla aligundua baba hayuko tena, aliachwa mikononi mwa bibi au nyanya.
Anasema binamu wake alimtishia kumuua ikiwa angetoboa siri iliyokuwa inaendelea mle nyumbani. Baada ya mazishi ya baba yake, baadhi ya ndugu za baba, mfano binamu wa baba na wajomba walianza kuishi kwao na kuendelea na masomo yao.
Celine anasema binamu huyo alikuwa na miaka kati ya 25-26 kitu kilichoanza, kama tabia ya binamu wa baba, kumtomasa kiliendelea kuwa kitendo cha kila siku cha unajisi na alimtishia kumuua ikiwa angetoboa siri iliyokuwa inaendelea mle nyumbani.
Anasema, hakujua wa kumgeukia, tabia yake ilibadilika mno na akawa msichana mtukutu na mwenye vituko. Hakuna mtu aliyeelewa, ni kwa nini alikuwa na tabia za usumbufu. Celine anasema alikuwa anaona aibu kumweleza mtu yeyote, hata bibi hakufahamu kuwa Celine alikuwa anapitia masaibu ya ubakaji kila siku.
Kitendo hicho kiliendelea tangu akiwa miaka minane hadi 14 hadi wakati binamu wake aliondoka kule nyumbani kwao na ilisalia kuwa siri.
Kushika Mimba
Celine alipohitimu miaka 15 alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana mmoja. Mwanadada huyu anasema kuwa kwa mara ya kwanza alihisi kupendwa, mara tu alishika mimba na akajifungua mtoto wa kwanza akiwa na miaka 16.
Maisha yalibadilika mno, alitelekezwa na walezi wake, na akaanza maisha ya malezi ya mtoto. Uhusiano wake na yule baba ya mtoto uliharibika wakati huo. Mtoto alipofikisha mwaka mmoja na miezi kadhaa Celine na yule mpenzi wake walirudia mapenzi tena na akiwa na miaka 17 alijipata ujauzito wa pili .
Kipindi hicho baba wa watoto wake wawili alifanikiwa kusafiri Marekani kwa ajira, lakini wakati huo alikuwa anatuma fedha za matumizi kwake Celine. Baada ya miaka miwili baba ya watoto alirejea kutoka Marekani, waliamua kuanza maisha kama mke na mume, na Celine alishika mimba ya tatu, ila mambo yalikuwa tofauti.
Mume wake alikuwa hajali, kwa mfano alikuwa na tabia ya kuwaleta wapenzi wengine ndani ya nyumba yao. Maisha ya kuwalea watoto wake hayakuwa rahisi na ndipo alihamia mtaani au kwenye nyumba ambazo hazina watu na, Februari alifunga ndoa na mume aliyekubali kuhudumia wanawe.
CREDIT: BBC
