×

Shigongo: Dkt. Tizeba Umefanya Jambo la Kishujaa – Video

ERIC SHIGONGO, mgombea ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),jana Ijumaa, Septemba 25, 2020, amezindua rasmi kampeni zake za kunadi sera zake na kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo ili waweze kumpa ridhaa ya kuwa mbunge kwa miaka mitano ijayo.

 

Akizungumza katika kampeni hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Nyakaliro, Shigongo alimshukuru aliyekuwa mshindani wake na mbunge aliyemaliza muda wake, Dkt. Charles Tizeba na kusema:

 

“Kura za maoni tulikuwa 34, ulikuwa mchakato mgumu, mrefu na wenye mateso, walioshiriki wanafahamu, kwa namna ya pekee.  Namshukuru sana Dkt. Charles Tizeba, alikuwa mshindani wangu, tulipambana kwelikweli lakini mwisho wa siku nikateuliwa kuipeperusha bendera ya CCM.  Alichokifanya hapa leo ni kitu kikubwa sana, kimenipa moyo, amekubali na kuamua kuniunga mkono.

 

“Namshuruku sana Dkt. Tizeba kwa kuja kuungana nami katika uzinduzi wa kampeni zangu, natambua juhudi kubwa na mambo makubwa aliyofanya kwa kipindi chake cha miaka kumi katika uongozi wa jimbo letu.  Nami nimuahidi endapo wananchi watanichagua, kwa kushirikiana na viongozi wenzangu na Serikali yangu nitayaenzi, kuyaendeleza pamoja na kufanya mengine makubwa zaidi kadri Mungu atakavyotujalia. Asante sana Tizeba, Mungu akubariki kaka,” amesema Shigongo.

 

Leave a Comment