×

Jiwe Kubwa la Madini Lapatikana Morogoro

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko, ametangaza habari njema baada ya kupatikana kwa jiwe jingine tena kubwa la madini aina ya spinel ambalo limepatikana kupitia kwa wachimbaji wa madini katika mgodi wa Mahenge mkoani Morogoro.

 

Biteko ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter; “Hongereni sana wachimbaji Mahenge, hili jiwe kubwa la Spinel limepatikana tena, JPM alisema ni wakati wenu, asanteni sana kwa kuchapa kazi.. JPM2020 #KaziIendelee”

 

Kwa kipindi cha miezi mitatu kumekuwa na manufaa makubwa na ongezeko la upatikanaji wa mawe ya madini.

 

Mchimbaji mdogo Saniniu Laizer ambaye Juni 24, 2020 aliishangaza dunia baada ya kuiuzia serikali madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 9.27 na kisha akapata jiwe la kilo 5.80 yaliyompatia mabilioni ya pesa.

Leave a Comment