MWANAJESHI wa kitengo maalum cha makombora, Alexey Alexandrov (35), amekiri kuwaua kwa pamoja warembo wawili, Ksenia Soltanova na Rafiki yake Natalia Kuznetsova, mwaka 2018 nchini Urusi akisema chanzo ni kulipa kisasi kwa kuonewa akiwa utotoni na si wivu wa kimapenzi kama wengi wanavyodai.
Alexey amesema utotoni akiwa nyumbani na hata shuleni alikuwa anaonewa sana na watu na aliapa kulipa kisasi. “Lengo langu lilikuwa kuua haijailishi ni nani ningemuua, niliwakuta warembo wanakula pizza nikawaua na miili yao nikaitupa kwenye nyasi na kwenda zangu nyumbani.
“Siyo kwamba hawa ndiyo ambao walinionea hapana, nilionewa na wengine kabisa ambao siwezi kujua wako wapi kwa sasa ila tu nilipanga siku moja nitaua, na muda ulipofika hawa ndiyo walikuwa mbele yangu nikamalizana nao,” alisema Alexey.
