×

Banana: Nashindana na Baba Kuimba, Hatumalizi Project – Video

MKALI wa sauti Bongo, Banana Zoro, amesema kuwa amekuwa kwenye ushindani mkubwa  na baba yake mzazi kiasi kwamba kila mmoja anatamani kufunika uwezo wa mwenzake, jambo ambalo limefanya hata project zao nyingi za pamoja kushindwa kukamilika.

Banana Zoro akiwa na DJ Big Dady ndani ya studio za +255 Global Radio.

Banana amesema hayo leo wakati akipiga story na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio kila Jumatatu hadi Ijumaa, saa 6:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni.

 

“Kwenye band yetu (B-Band) tunafanya na baba yangu Mzee Zoro lakini inategemeana na mteja anataka nini, anaweza kutaka band pamoja na mimi niimbe, au akataka baba ndiye apafomu ama wote. Kwa hiyo tupo na tunapiga kazi.

…Akiwa na mtangazaji, Dar Boy, ndani ya studio za +255 Global Radio.

“Band yetu ni muunganiko wa wasanii lakini mimi ndiyo niliianzisha na yote ipo chini ya record label ya Muziki ya Miziki, wapo wasanii kibao ambao tunafanya nao kazi.

“Siwezi kujutia kumweka dada yangu Maunda Zoro kwenye ramani kwa sababu mambo yanabadilika, sisi mzee alituandalia mazingira mapema, ukiwa staa halafu mambo yako yakawa siyo poa inakuwa shida kidogo.

“Mimi na Mzee Zoro tuna ushindani mkubwa sana, huwa tunafanya project za kolabo lakini hatujawahi kumaliza kwa sababu kila mmoja anataka kumfunika mwenzake mpaka wimbo unaharibika.

…Akiwa na mtangazaji, Stewart George, ndani ya studio za +255 Global Radio.

“Mimi na Nuruel tunakutana sana, tunawasiliana sana, nikifanya kazi na mtu hata kama tukiwa mbali baada ya miaka kadhaa hawezi kuwa rafiki yangu labda yeye mwenyewe aamue.

“Nina kazi nyingi sana na Mrisho Mpoto na wasanii wengine ambazo tunafanya studio kila siku, Watanzania wakae tayari muda wowote, tunaachia kitu,” amesema Banana.

 

Leave a Comment