IMERIPOTIWA kuwa mwanamuziki Nicki Minaj na mpenzi wake, Kenneth Petty, wamepata mtoto wao wa kwanza baada ya Nicki kujifungua siku ya jana huko Los Angeles.
Nicki ali-share kwa mara ya kwanza kuwa ni mjamzito na anatarajia mtoto mwezi wa Julai mwaka huu. Pamoja na ku-post picha zake akiwa mjamzito kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo, mpaka sasa bado jinsia wala jina la mtoto huyo havijawekwa wazi.
