×

Trump, Mkewe Wakutwa na Corona

RAIS Donald Trump wa Marekani amesema  yeye na mke wake, Melania Trump, wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.

 

Tump ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter, hii ni baada ya wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

 

Bi Hope Hicks, 31, ambaye ni  mshauri  na msaidizi wa karibu wa Trump, alisafiri na Trump kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii.

 

Baadaye jana  Alhamisi,  Trump alisema yeye na mke wake wanajiweka karantini baada ya Bi. Hicks kuthibitishwa kuwa na corona.

 

Leave a Comment