Waliojishindia Mkwanjwa wa Chemshabongo ya Gazeti la Ijumaa Wakabidhiwa Zawadi Zao
Global Publishers March 6, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Mshindi wa Chemshabongo ya Gazeti la Ijuma aliyejibu swali kwa ufasaha na kujishindia Tsh. 30,000, Rukia Kassim ambaye ni mkazi wa Miembe Saba Kibaha-Pwani akionesha mkwanja wake baada ya kukabidhiwa.Mhariri wa Gazeti la Risasa, Erick Evarist (kushoto) akimkabidhi Mshindi wa Chemshabongo ya Gazeti la Ijuma aliyejibu swali kwa ufasaha na kujishindia Tsh. 30,000, Salma Juma ambaye ni mkazi wa Kisarawe-Pwani.Mkuu wa Kitengo Cha Masoko Cha Global Group, Adam Anthony (kushoto) akimkabidhi Mshindi wa Chemshabongo ya Gazeti la Ijuma aliyejibu swali kwa ufasaha na kujishindia Tsh. 30,000, Rukia Kassim ambaye ni mkazi wa Kibaha.Mhariri wa Gazeti la Risasa, Erick Evarist (kushoto) akimkabidhi, Rukia Kassim Fulana ya Ijumaa Mshindi wa Chemshabongo ya Gazeti la Ijuma aliyejibu swali kwa ufasaha.Mshindi wa Chemshabongo ya Gazeti la Ijuma, Salma Juma ambaye ni mkazi wa Kisarawe-Pwani. aliyejibu swali kwa ufasaha akionesha mkwanja aliokabidhiwa.
Ikiwa ni wiki nyingine tena kwa wale wasomaji wetu wa Gazeti la Ijumaa kuendelea kujinyakulia zawadi zao kupitia chemshabongo ambapo msomaji wa gazeti hilo hujibu swali lililo katika ukurasa wa pili na kujishindia mkwanja wa Tsh.30,000 elfu ambapo leo wamekabidhiwa.
Akizungumza Mhariri wa Gazeti la Risasi kwa niaba ya Mhariri wa Gazeti la Ijumaa,Erick Evarist amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa kila wiki kwa wasomaji wa gazeti hilo kuendelea kujinyakulia mkwanja kupitia chemshabongo iliyopo ukurasa wa pili na wasomaji waendelee kulinunua kwa wingi ili wawe miongoni mwa washindi.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Usambazaji cha Global Group, Anthony Adam ameshuhudia washindi hao wakipewa mikwaja yao na amekazi tena na neno lake la kwamba mwendo ni uleule kwa wiki ijayo ambao watanunua gazeti la Ijumaa watanufaika na zawadi mbalimbali zinazoendelea kutolewa.