×

Rais JPM Apokea Utambulisho wa Mabalozi – Video

RAIS John Magufuli, leo Jumatatu, Oktoba 5, 2020, amepokea hati za utambulisho wa mabalozi wa Marekani na Vietnam nchini.

 

Mabalozi hao ni Nguyen Nam Tien Balozi Vietnam na Donald John Uright wa Marekani na Balozi wa Pakistan.

 

Balozi wa Pakistan hapa nchini Mohamed Salim amesema ataweka juhudi zaidi katika uwekezaji na kujenga uwezo ili kuimarisha mahusiano ya nchi yake na Tanzania.

Balozi Salim amebainisha hayo alipoanza majukumu yake rasmi kama balozi kamili mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais Magufuli, muda mfupi uliopita Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema nchi ya Pakistan ina wawekezaji wa kutosha hivyo atasaidia wafanyabiashara wa kitanzania kuuza bidhaa zao nchini humo.

 

Leave a Comment