KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas leo Oktoba 6, 2020, ameshiriki uzinduzi wa jezi mpya za timu ya taifa (Taifa Stars) uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo pia Kampuni ya Bia ya Serengeti imeongeza mkataba wake wa udhamini kwa timu ya taifa wenye thamani ya shilingi bilioni 3.



