VICHWA vya habari vikubwa vimezidi kumfuata staa wa muziki Tanzania na Barani Afrika kwa jumla, Diamond Platnumz, baada ya kufanyiwa mahojiano maalumu na waandaaji wa tuzo kubwa duniani za muziki — GRAMMYs.
Kupitia website yao pamoja na kurasa zao za mitandao ya kijamii, Grammy wamemuelezea Diamond kama mwanamuziki aliyeweza kubadilisha taswira ya muziki wa Afrika Mashariki pamoja na kufikia viwango ambavyo ni ndoto ya kila mwanamuziki kufika.
Grammys pia wamesifu jitahada za Diamond kwa kuweza kuongezea ladha za muziki kwa lugha za Kiingereza na Kiswahili, taarabu, R&B na Caribbean, nyimbo za slow na za kishisia katika muziki wa “BongoFleva”, kitu kilichofanya aweze kuvuka mipaka tofauti na watangulizi wake ambao wametajwa kuwa ni Dully Sykes, Juma Nature, TID na Q Chief.
Haya ni baadhi ya mambo yaliyomfanya kutusua kimuziki na kufanikiwa kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani kama vile Omarion (“African Beauty”), Rick Ross (“Waka”), Ne-Yo (“Marry You”) and most recently, Alicia Keys (“Wasted Energy”).
Tuzo za Grammys ndizo Tuzo kubwa zaidi za muziki duniani na ndoto ya kila mwanamuziki! Hivyo kitendo cha waandaaji wa tuzo hizi kumzunguzia na kumpa heshima Diamond, ni ishara nzuri kwa muziki wa Afrika Mashartki.
Grammy wameendelea kutaja ngoma za Mondi zilizotikisa zaidi ni; Number One, Kamwambie, Kidogo, Sikomi, Inama, Baba Lao, Nana na Jeje.

