×

Morrison, Mugalu Wateketeza Mamilioni

MASTAA 22, wanaounda kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara klabu ya Simba wakiwemo, Benard Morrison na Chris Mugalu pamoja na viongozi 11 walioambatana nao wameteketeza mamilioni ndani ya siku tatu tu ambazo walikuwepo jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania.

 

Huko Dodoma, Simba ilifi kia kwenye hoteli kubwa na ya kifahari yenye hadhi ya nyota tatu inayojulikana kama, Morena Hotel iliyopo Medeli West inayotoa huduma mbalimbali.

 

Unaambiwa gharama ya kulala usiku mmoja tu kwenye vyumba vya kawaida ni shilingi 106,000 kwa chumba cha mtu mmoja ‘Single’ huku vile vya watu wawili ‘Double’ vikiwa na gharama ya Shilingi 108,000/= Simba imesafi ri na msafara wa watu 33 ambapo 11 kati yao ni benchi la ufundi linaloongozwa na kocha, Sven Vandenbroeck pamoja na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo huku wachezaji wanaounda kikosi hicho wakiwa ni 22.

 

Kwa kawaida viongozi wa timu hiyo wanaposafi ri hutumia vyumba vya mtu mmoja ‘Single’ wakati wachezaji wao hutumia vyumba vya watu wawili ‘Double’ hivyo kama utapiga hesabu kwa gharama ya vyumba pekee ukiachana na mahitaji mengine kwa siku tatu ambazo kikosi hicho kimekaa ndani ya hoteli ya Morena kitakuwa kimeteketeza zaidi ya Shilingi Milioni 7,062,000/=.

 

Kabla ya mchezo wa jana Simba ilikuwa ikikamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 10.

SAID ALLY NA JOEL THOMAS

Leave a Comment