×

Mapokezi ya Shigongo Magulukenda Balaa – Pichaz

MAPOKEZI ya mgombea ubunge Jimbo la Buchosa, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo Jams, katika Kijiji cha Magulukenda, Kata ya Kalebezo, yametikisa alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji hicho jana.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Shigongo amesema changamoto zilizopo katika kijiji hicho atazitatua kwa kushirikiana na wananchi ikiwa ni pamoja na wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kama ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule za msingi na sekondari.

Mengine ni zahanati, barabara na shughuli zingine za kijamii ambazo zitahitaji nguvu ya wananchi, jambo ambalo litasaidia kufikia malengo ya maendeleo katika jimbo hilo.

Shigongo anaendelea na kampeni zake jimboni Buchosa akinadi sera za chama chake cha CCM pamoja kuwaomba ridhaa wananchi ili wawachague viongozi wa CCM kuanzia kiti cha urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

Leave a Comment