×

Shigongo Aahidi Kuipaisha Michezo Buchosa

MGOMBEA wa kiti cha Ubunge jimbo la Buchosa kupitia kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),  Eric Shigongo, ameweka wazi kuwa, endapo wananichi wa jimbo hilo watampa ridhaa ya kuwaongoza Oktoba 28 mwaka huu, atahakikisha anaipaisha michezo jimboni hapo.

 

Shigongo ameyasema hayo kwenye mikutano yake ya kampeni aliyoifanya kwenye vijiji vya Katwe, Chema, Bilulumo, Ruhorongoma na Kafunzo, ambapo aweka wazi kua ataanzisha michuoano yake ya Shigongo Cup, ili kuzifanya timu zote za jimbo hilo kushiriki.

 

Akizungumza mbele ya wapiga kura wake Shigongo alisistiza kwamba endapo wakazi wa jimbo hilo watamchagua basi atatumia fursa hiyo ya michezo kuwaunganisha wakazi wote wa jimbo hilo kutokomeza wimbi la ubaguzi wa makabira na ukanda.

 

“Naomba kutumia fursa hii kwenu wakazi wa kafunzo kuwaahidi kuwa, endapo Oktoba 28 mwaka huu mtanipa kura nyingi mimi na Rais John Pombe Magufuli na madiwani wote wa kata hii, basi mfahamu kuwa changamoto zote za mabarabara, elimu, umeme na uvuvi zinaenda kufutika.

 

“Naimani kuwa naenda kumaliza kero hizo za miundo mbinu kwa sababu nitanunua Katapila langu kwa ajili ya kutengeneza barabara zote za jimboni kwangu, ila pia irani yetu ya uchanguzi imejipambanua juu ya uboreshaki wa huduma za afya, umeme na elimu jambo ambalomimi nitaenda kuibana serikali ili iweze kutimiza kwa wakati.

 

“Ninachowaomba kwa sasa no kuhakikisha mnamipa kura nyingi mimi na madiwa pamoja na Rais Magufuliili nikatimize haya kwa haraka na kwamba msinichanganyie madiwani nje ya CCM, maana nafahamu kuna watu wanataka kutuharibia kura zetu ili nionekane sikushinda kwa kishindo baadae waje kugombea wao,” alisema Shigongo.

Stori na Musa Mateja | GPL

Leave a Comment