×

Nigeria: Davido Aongoza Maandamano Dhidi ya Polisi

NYOTA wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke (Davido),  ameongoza sehemu ya maandamano ya vijana nchini humo kutaka kufutwa kwa Kikosi Maalumu cha Polisi cha Kupambana na Uhalifu (SARS), kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya raia wa nchi hiyo hasa vijana.

 

Mitaa katika majiji makubwa ya Nigeria, Ijumaa iliyopita ilijaa vijana wenye hasira wakiwa na mabango yenye maandishi mbalimbali yakiwemo yasemayo #ENDSARS. Hashtag ya Endsars nayo ina-trend mtandaoni kwa zaidi ya wiki moja sasa

Serikali ya Nigeria imevunjilia mbali kikosi chake maalum cha polisi baada ya maandamano ya umma kutokana na madai ya ukatili wa polisi na itafanya uchunguzi kuhusu shughuli za kikosi hicho. Hayo yametangazwa leo na ofisi ya urais nchini humo.

Ujumbe wa ofisi hiyo kupitia mtandao twitter, unasema kuwa kikosi maalumu cha kukabiliana na waporaji kinachojulikana kama SARS kimevunjiliwa mbali mara moja.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, jeshi la polisi nchini humo limetangaza kufanya uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu uliotendwa dhidi ya raia na kuongeza kuwa waliohusika watachukuliwa hatua.

 

Awali huku maandamano hayo yakitarajiwa kuwa ya amani, waandamanaji walishambulia kituo cha polisi na kusababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi. Polisi walifyatua gesi za kutoa machozi na pia kuwarushia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji hao ambao waliwashtumu maafisa hao kwa kutumia risasi za moto.

 

Leave a Comment