×

Lissu Aendelea na Kampeni Singida

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,( Chadema), Tundu Lissu, amewataka wananchi kuchagua serikali itakayosimamia haki, uhuru na maendeleo ya watu.

 

Akizungumza jana Oktoba 11,2020, katika kampeni zake zilizofanyika katika eneo la Iguguno, Iramba Mashariki, mkoani Singida, mgombea huyo amewataka wananchi hao kuacha kulalamika badala yake wachukue hatua ili waweze kupata maendeleo yenye maana kwao.

 

‘’Kama unataka kuwa huru kuuza biashara zako ukiwa huru, uuze chochote unachozalisha ukiwa huru chagua Tundu Lissu. Mtoto wako akienda shuleni au hospitali atendewe haki na si kununua haki, mama lishe atendewe haki na bodaboda atendewe haki,’’ alisema Lissu.

 

Aidha, Lissu amesema kuwa hata kwenye maandiko matakatifu yameandika haki huinua taifa,  hivyo taifa litainuka kukiwa na haki na tukiwa huru.

Leave a Comment