×

Rais JPM Sasa Napandisha Mishahara – Video

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli, leo Oktoba 20, 2020, amefanya mkutano katika uwanja wa TTC Korogwe mkoa wa Tanga leo na kunadi sera za chama hicho na kuomba ridhaa ya wana CCM, na wananchi kumchagua kuwa Rais na kuchagua wabunge na madiwani wa CCM.

 

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Dkt. Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa watumishi iwapo atapewa ridhaa hiyo huku akisisitiza wananchi kutunza amani wakati huu wa uchaguzi kwani nchi ikivurugika Taifa litaingia kwenye matatizo.

“Miaka mitano iliyopita, tumeajiri watumishi 74,000, tumeimarisha uchumi wetu, sasa miaka mitano ijayo tutakuwa na jukumu la kuongeza mishahara, huwezi kupandisha mishahara wakati huna uchumi, wengine wanazungumza tu hawajawahi kutawala, hata kujenga ofisi za chama zimewashinda.

“Katika miaka mitano iliyopita tumetekeleza miradi 64 ya maji katika Mkoa wa Tanga, huku 54 ikiwa vijijini na 10 iko mjini, miongoni mwao ni mradi wa Pongwe, Muheza, tumetekeleza miradi 64 ya maji katika Mkoa wa Tanga, huku 54 ikiwa vijijini na 10 iko mjini, miongoni mwao ni mradi wa Pongwe, Muheza.

Yaani kutoa elimu bure, kupeleka umeme vijijini, kujenga vituo vya afya, kutoa mikopo kwa wanafunzi vyuo vikuu, kujenga SGR, kujenga bwawa la Umeme yote haya nimefanya makosa hadi msinirudishe miaka mitano mingine wana Korogwe?

Ninawasihi vijana wetu, anakuja mtu anawahamasisha kwa faida yake, kiko chama kwenye ilani yao, kimezungumza kikipewa ridhaa, kitaweka rehani madini. Ukiweka rehani madini utasomesha sangapi watoto, utapata wapi fedha za kujenga reli.,” amesema Magufuli.

 

Leave a Comment