×

Man United Wababe wa PSG

MANCHESTER United usiku wa jana   kwa mara nyingine wamefanikiwa kuchukua pointi tatu kutokea jiji la Paris Ufaransa baada ya kuwafunga wenyeji wa PSG katika ardhi ya kwao katika uwanja wa Parc de Prince huu ukiwa ni mwanzo mzuri wa kuanza kushindania ubingwa wa Uefa Champions League.

Kwenye mchezo huo Man United waliamua kuwaacha PSG wamiliki mpira  na pindi walipoupata mpira walikuwa wanafanya mashambulizi ya kushtukiza (counter attacks) ambazo zilionekana kuwapa shida PSG, na kama Marcus Rashford na Anthony Martial wangekuwa makini wangeondoka na ushindi mnono zaidi.

Magoli ya Man United yaliwekwa nyavuni na nahodha wao wa mchezo, Bruno Fernandes, dakika ya 27 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 87 Marcus Rashford akafunga goli la ushindi kwa Man United ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa Kundi H.

Kwenye mchezo huo, licha ya Anthony Martial kujifunga na kuwafanya PSG waweze kusawazisha dakika ya 55, Man United wameibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 2-1 na wanaongoza kundi H sawa na RB Leipzig kwa pointi tatu.

 

 

Leave a Comment