MSIMAMIZI wa uchaguzi katika Jimbo la Tarime Vijijini amemtangaza Mwita Waitara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 35,758 akifuatiwa na John Heche wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyepata kura 18,757.
