MUSWADA tata wa kikatiba ulishindwa kupitishwa bungeni jana Oktoba 29, 2020 kufuatia upinzani mkali kutoka kwa asasi za kiraia na vyama vingine vya siasa.
Wabunge waliopiga kura kuunga mkono muswada huo uliopewa jina la ‘Bill 10’ walikuwa 105, na zilikosekana kura sita pekee kupata theluthi mbili ya kura ambazo ni 111.
Endapo ungepitishwa, ungeongeza mamlaka ya kuteua majaji na mawaziri pamoja na kuruhusu mabadiliko kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu.
Baada ya kushindwa kwa muswada huo, Waziri wa Sheria, Given Lubinda, amesema jambo hilo ni changamoto ya muda mfupi.
Zambia inategemewa kufanya uchaguzi mkuu mwaka 2021.
