MSANII wa Hip Hop Bongo, Abdulaziz Chende ‘Janjaro’ amefunguka kuwa, kwa sasa mpango wa kutafuta mtoto bado sana maana anajipanga na hawezi kukurupuka.
Janjaro ambaye yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo wa Arusha ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa jijini humo, amesema kwa sasa wanakula bata kwanza wakiendelea kutathmini siku wakipata mtoto wao ataishije.
“Huwezi kuzaa kwa ajili ya watu, sina mpango wa kuwa na watoto zaidi ya watatu, nadhani wawili wananitosha, lazima nijipange kwanza kujua mwanangu ataishije nisije nikakurupukia kuzaa halafu mwanangu akateseka,” anasema Janjaro.
STORI: KHADIJA BAKARI, DAR
